MAHAKAMA YAMTOA LULU GEREZANI

Muigizaji wa filamu nchini Elizabeth Michael, maarufu Lulu, amebadilishiwa adhabu na sasa anatumikia kifungo cha nje kwa amri ya Mahakama Kuu Tanzania.

Ofisa Habari wa Jeshi la Magereza, Lucas Mboje amesema Lulu amebadilishiwa adhabu na ameachiwa juzi Jumamosi kati ya saa 2 hadi 3 asubuhi.

Mboje alisema kuwa si kwamba ameachiwa huru, bali amebadilishiwa adhabu na atatumikia kifungo cha nje, kitaalamu tunaita ' Community service'.

Lulu alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela Novemba mwaka jana baada ya kupatikana na hatia ya kumuua bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Kanumba.

No comments