TFF YAIPIGIA UPATU YANGA KUELEKEA KATIKA MECHI DHIDI YA TP MAZEMBE



Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF limewataka watanzania kwa ujumla kwa pamoja kuendelea kuiunga mkono timu ya Yanga katika ushiriki wake kwenye michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika

Ofsa Habari wa TFF,Alfred Lucas amesema kwamba licha ya timu hiyo kuanza vibaya kwenye kampeni zake hizo kwa kuweza kufungwa bao 1-0 dhidi ya Mo Bejaia ya nchini Algeria lkn wana nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwenye michuano hiyo hasa kufuatia mfumo uliopo wa hatua ya makundi

Amesema kwamba kwa sasa ni vyema kila mmoja akaipa sapoti timu hiyo kwani ni timu pekee kwenye ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati ambayo imesalia kwenye michuano ya kimataifa kwa ngazi ya vilabu

No comments