BAADA YA DORNAD NGOMA NA AMISI TAMBWE KUGOMBANA WAKIWA KAMBINI,,UONGOZI WA YANGA WATOA UFAFANUZI JUU YA SWALA HILO


Uongozi wa timu ya Yanga umesema kwamba hakuna malumbano yeyote yanayowahusu wachezaji wao Amisi Tambwe pamoja na Dornad Ngoma juu ya wachezaji wao kutoelewana mara baada ya wawili hao kuzozana wakiwa kambini huko nchini Uturuki

Mkuu wa mawasiliano wa klabu hiyo Jerry Muro amesema kwamba kwa sasa wachezaji hao wameshamaliza tofauti zao na kila mmoja anaelekeza nguvu zake kuisaidia timu

Amesema kwamba jambo hilo la kukwaruzana kwa wachezaji hao lilitokea wakiwa mazoezini mara baada ya mmoja wa wachezaji hao kumfanyia mazambi mchezaji mwenzake lkn kocha mkuu sambamba na viongozi wamezungumza nao na kuondoa tofauti zao

Hata hivyo amesema kwamba kutokana na morali waliyo nayo wachezaji wakiwa mazoezini hua inasababisha kutokea mambo kama hayo hivyo ni vyema watanzania wakalifahamu jambo hilo.

No comments