JUMA NDAMBILE ASEMA YUPO TAYARI KUMSAIDIA TENA IBRAHIMU HAJIBU MIGOMBA KATIKA SAFARI YAKE YA KUCHEZA SOKA LA KULIPWA


Aliyekua meneja wa mshambuliaji wa klabu ya Simba Ibrahim Ajib Migomba, Juma Ndambile amesema bado ana nafasi nyingine ya kumsaidia mchezaji huyo endapo viongozi wa Msimbazi wataridhia ombi la kumruhusu kucheza soka la kulipwa nchini Afrika kusini.

Ndambile amesema dhamira yake ni kumsaidia mshambuliaji huyo na ndio maana alibeba jukumu la kumpeleka Afrika kusini kufanya majaribio katika klabu ya Golden Arrows lakini tabia za uongo za Ajib zilimkatisha tamaa.

Hata hivyo amedai kwamba Ajib alikua ameshapata nafasi yakubadilisha mazingira ya soka lake, na kwa sasa huenda angekau katika maandalizi ya kuelekea Afrika kusini, lakini mambo yamekua tofauti.

No comments