COASTAL UNION WASEMA JUMA MAHADHI YUKO HURU KUICHEZEA YANGA


Uongozi wa timu ya soka ya Coastal Union ya mkoani Tanga umesema kwamba kwa sasa upo kwenye mazungumzo na uongozi wa timu ya soka ya Yanga juu ya swala la mchezaji Juma Mahadhi kuitumikia timu hiyo kwenye michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika

Kaimu katibu mkuu wa klabu hiyo,Salum Bawazili amesema kwamba mchezaji huyo kwa sasa tayari ameshamaliza mkataba wake na klabu hiyo ya mkoani Tanga hivyo kwa sasa wanaangalia namna ya kuwapa barua Yanga juu ya idhini ya kumalizana na mchezaji huyo

Amesema kwamba kwa sasa wanaendelea na mazungumzo na katibu mkuu wa klabu hiyo hivyo ana imani jambo hilo litakamilika mapema ili kuweza kufanikisha mchezaji huyo anaitumikia timu yake hiyo mpya

No comments