JUMA ABDUL AWAOMBA VIONGOZI WA SIMBA WAMRUHUSU HASSANI KESSY AITUMIKIE YANGA


Beki wa pembeni wa klabu ya Young Africans Juma Abdul Jaffar, amewataka viongozi wa klabu ya Simba kulegeza kamba kwa kukubali kutoa ruhusa kwa beki mwenzake Hassan Kessy ili aanze kuitumikia klabu yake mpya katika michuano ya kimataifa.
 
Juma Abdul ambaye tayari ameshakosa mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika CAF, amesema kuna haja ya jambo hilo kumalizwa ili kuondoa utata uliozua sintofahamu mingoni mwa wadau wa soka nchini kote.
 
Amesema Simba wanapaswa kufikiria uzito wa michuano ambayo Young Africans wanashiriki kwa sasa ikiwa ni pamoja na kuziweka pembeni tofauti za kiitikadi, ili kumsaidia Kessy kutimiza ndoto yake ya kucheza soka la kimataifa.

No comments