HOFU YA KUKATIKA KWA UMEME YANGA YAAMUA KUSITISHA MPANGO WA KUCHEZA MECHI USIKU


Mchezo wa kombe la shirikisho barani Afrika kati ya Yanga dhidi ya TP MAZEMBE sasa rasmi utapigwa siku ya jumanne ya tarehe 28 ya mwezi kunako majira ya saa kumi kamili za jioni

Awali kumekua na taarifa kwamba mechi hiyo huenda ingepigwa siku ya jumatano majira ya saa moja na nusu usiku ili kuweza kuwapa fursa waumini walio kwenye mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani kupata muda wa kutosha wa kushuhudia pambano hilo sambamba na watu walio makazini nao kupata muda wa kuutazama mpambano huo

Mkuu wa mawasiliano wa klabu hiyo Jerry Cornel Muro amesema kwamba sababu kubwa ambayo imepelekea mechi isipigwe siku ya jumatano majira ya usiku ni kutokana na jenereta ya uwanja wa Taifa kutokua kwenye hali ya kufanya kazi


No comments