YANGA WAKUBALIANA NA MATOKEO YA KUFUNGWA NA MO BEJAIA,
WAVUNJA SAFARI YA KUREJEA NCHINI UTURUKI
JERRY MURO MKUU WA MAWASILIANO WA YANGA
Uongozi wa mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara timu ya soka ya Yanga umesema kwamba kwa upande wao wameyapokea matokeo yaliyotokea katika mchezo wao dhidi ya Mo Bejaia ya nchini Algeria ambapo mabingwa hao walikubali kupokea kipigo cha bao 1-0 wakiwa ugenini

Mkuu wa Habari wa timu hiyo Jerry Murro amesema kwamba japo mazingira ya mchezo hayakua mazuri lkn wanakubaliana na matokeo hayo kwani goli ambalo wamefungwa lilikua halina kikwazo
Amesema kwamba wakati wowote kuanzia sasa kikosi kitarejea hapa nchini tayari kujiandaa na mechi inayofuata dhidi ya timu ya TP Mazembe
Murro amedai kua timu itarejea hapa nyumbani na hawana mpango wa kwenda nchini Uturuki kuweka kamba ksb mechi hiyo itapigwa hapa nyumbani hivyo hakuna haja ya kuweka kambi sehemu hiyo
Hata hivyo amewataka mashabiki wa timu hiyo kuwa pamoja katika kipindi hiki ambacho ni muhimu kuonyesha ushirikiano wa kutosha ili kikosi cha timu hiyo kiweze kufanya vizuri kwenye michuano hiyo
Post a Comment