TP MAZEMBE YAPATA PIGO,MMILIKI WA KLABU HIYO ATUPWA JELEA KWA MIAKA MITATU


Mmiliki wa timu ya TP MAZEMBE,Moise Katumbi amehukumiwa kwenda jela kwa miezi 36 sawa na miaka mitatu na kupigwa faini ya dola 6,000,000 sawa na bilioni 12 baada ya kukutwa na hatia ya kujimikilikisha jengo baada ya kufoji saini

Katumbi anakumbana na adhabu hiyo huku akiwa ameingia katika harakati za kisiasa za kuwania nafasi ya Raisi wa DRC huku ikiaminika ni mmoja ya watu ambao anaungwa mkono na baadhi ya vyama vya upinzani

Ikikumbukwe kua  mmiliki huyo wa timu ya TP MAZEMBE anakumbana na adha hiyo huku timu yake ikitarajiwa kucheza na mabingwa wa Tanzania bara timu ya Yanga katika mchezo wa kombe la shirikisho barani Afrika mechi inayotarajiwa kupigwa siku ya jumanne ya tarehe 28 ya mwezi huu

Awali kumekua na taarifa kwamba timu ya TP MAZEMBE imeshindwa kufanya vizuri katika michuano ya kilabu bingwa barani Afrika kutokana na kiongozi huyo kujikita kwenye siasa hivyo hatua hii ambayo imetokea huenda ikawa pigo kubwa kwa klabu hiyo hasa kwenye ushiriki wa michuano ya kombe la shirikisho

No comments