TP MAZEMBE KUTUA NCHINI SIKU YA JUMAPILI KUWAKABILI YANGA


Kikosi cha timu ya TP MAZEMBE kinataraji kuwasili hapa nchini kikiwa na jumla ya msafara wa watu 32 kwa ajili ya mchezo wa kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya Yanga mechi ambayo inataraji kupigwa siku ya jumanne ya tarehe 28 ya mwezi huu

Ofsa Habari wa TFF,Alfred Lucas amesema kwamba mara baada ya kuwasili msafara huo unatarajiwa kufikia katika  Hoteli ya Serena ambayo ina sifa ya kuwa na nyota tano

Hata hivyo Lucas ameendelea kuwatahadharisha viongozi wa Yanga kuwa makini na mashabiki wao kuelekea kwenye pambano hilo ili kusije kuleta athari kwa timu hiyo hasa kwenye ushiriki wa michuano hiyo

Amesema kwamba shirikisho hilo limepata taarifa kutoka kwa baadhi ya mashabiki wa Yanga kua wana mpango wa kukaa kwenye jukwaa ambalo hua wanakaa mashabiki wa Simba,hivyo jambo hilo linaweza kuleta vurugu kwa mashabiki hao

Aidha amedai kua mfano mzuri ni ule ambao umeikumba timu ya ES Setif ya Algeria
ambapo CAF imeiondoa kwenye mashindano mara baada ya mashabiki wake kufanya vurugu kubwa katika mchezo wake wa klabu bingwa barani Afrika dhidi ya timu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini 

No comments