TYSON FURY ANAFAA KUPIGWA MARUFUKU;ASEMA KLITSCHKO
Bondia wa uzani mzito duniani Tyson
Fury anafaa kupigwa marufuku katika mchezo wa ndondi kwa matamshi yake
ambayo yanamfananisha na Hitler,Wladimiri Klitschko amesema
.
Fury
aliomba msamaha mwezi uliopita baada ya kuchapisha kanda ya video
mtandaoni ilio na ubaguzi,ujinsia na maneno yanayokashifu Wayahudi.Lakini bingwa wa zamani katika uzani huo Wladmir Klischko ambaye atakabiliana na Fury mjini Manchester tarehe 9 mwezi Julai ,alisema: nilishangazwa na taarifa yake.
Wakati alipokuwa akiongea kuhusu Wayahudi alizungumza kama Hitler.''Mtu huyu ni mpumbavu''.
Raia huyo wa Ukrain ambaye alipoteza kwa Fury mnamo mwezi Novemba na hivyobasi kupoteza kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 11 aliongezea,''hatuwezi kuwa na bingwa kama huyu''.
''Ni lazima anyamazishwe ama anyamazishwe katika ulingo wa ndondi,kwa sababu huwezi kuongeza chuki zaidi ''Ninapigana na mtu ambaye hawezi kufunga mdomo kuhusu maswala fulani''.
Post a Comment