LIPULI FC WASEMA ASANTE KWASI HAENDI KOKOTE

Na Said Ally
Uongozi wa klabu ya Lipuli FC umesema kwamba hawautambui usajili uliofanywa na klabu ya Simba juu ya mchezaji wao Asante Kwasi licha ya taarifa kueleza kuwa mchezaji huyo amesaini kandarasi ya kuitumikia Simba.

Mwenyekiti wa timu ya Lipuli FC,Ramadhan Mahano ameiambia MWANDIKE.BLOGSPOT kwamba wao wanatambua kuwa Kwasi bado ni mchezaji wao na kesho anahitajika kujiunga na wenzake kwa ajili ya kuendelea na maandalizi ya michezo ya ligi kuu ya Tanzania bara.

Mahano alisema kwamba uongozi ulimpa ruhusa Kwasi baada ya kupatwa na msiba wa baba yake ambapo ruhusa hiyo inamalizika leo hii siku ya jumamosi.

"Sisi tulikuwa tunasubili mpaka jana kama kuna timu ambayo inamtaka Kwasi ingeweza kufika Iringa au tungewasiliana nayo ili kuweza kufanya taratibu hizo,lakini hadi jana dirisha la usajili linafungwa hakukuwa na klabu ambayo iliwasilisha ofa kwa ajili ya kutaka kumsajili mchezaji huyo"alisema Mahano.

Alisema kwamba kwa taratibu za usajili Kwasi haruhusiwi kufanya mazungumzo na klabu yeyote kwani mkataba wake haumruhusu kufanya mazungumzo na klabu nyingine kwani bado ana mkataba wa zaidi ya miezi wa kuendelea kuitumikia timu hiyo.

Aliongeza kusema kuwa mkataba wa mchezaji huyo utafikia ukiongoni ifikapo tarehe 28 mwezi wa saba katika mwaka wa 2018 baada ya kusaini mkataba huo july 29 mwaka huu.

Hata hivyo alisema kwamba endapo kama klabu ya Simba itawasilisha jina lake kunako TFF kwa upande wao watapeleka pingamizi TFF juu ya swala hilo kwani awali walishaanza kupeleka malalamiko yao TFF wakipinga baadhi ya klabu kuvunja taratibu za usajili.

No comments