KILIMANJARO STARS KUREJEA LEO HII

Na Said Ally
Mara baada ya kukamilika kwa mchezo wa kombe la Challenge kati ya Kilimanjaro Stars na Kenya,kikosi cha timu ya Tanzania bara kinataraji kurejea jijini Dar es salaam leo hii kwa ajili ya kuendelea na majukumu mengine.

Afisa Habari wa TFF,Alfred Lucas alisema kwamba,kikosi hicho kinarejea mapema ili wachezaji wawai kujiunga na timu zao ili wajiandae na michuano ya kombe la FA.

Kilimanjaro Stars imeshindwa kufanya vizuri katika michuano ya kombe la Challenge hivyo imejikuta ikitolewa mapema katika hatua ya makundi.

No comments