PIERE-EMERICK AUBAMEYANG HAKAMATIKI

NA FREDY REUBEN
Nyota wa klabu ya Borussia Dortmund Piere -Emerick Aubameyang amevunja rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote kutoka  Africa akiipiku rekodi hiyo iliyowekwa na Raia wa Ghana Anthony Yeboah iliyodumu kwa takribani miaka 22 aliezifumania nyavu mara 96 ndani ya Bundesliga.

Aubameyang amevunja rekodi ya Anthony Yeboah Mshambuliaji  wa zamani wa Eintracht Frankfurt na kuwa mchezaji mwenye magoli mengi kwenye hiatoria ya  ligi ya Bundesliga anaetoka Africa baada ya kufunga goli katika mchezo wao dhidi ya Werder Bremen hapo Jana.

Mshambuliaji wa Gabon ambae msimu uliomalizika alichukua kiatu cha Dhahabu katika ligi ya Bundesliga baada ya kuzifumania nyavu mara 31 huku akimuacha goli moja mbele mpinzani wake mkubwa Robert Lewandowski ilimsaidia kwa kiasi kikubwa na sasa amekuwa mfungaji wa muda wote kwenye ligi ya ujerumani.

Mchezaji bora wa mwaka wa Africa mwaka 2015 alikuwa na ukame  kidogo wa magoli kwani alikuwa hajafunga goli tangu walipocheza mzunguko wa nane wa ligi hiyo  pale walipopoteza kwa kufungwa goli 3-2 na RB Leipzig kabla ya kuja kuamka kwenye mchezo wao wa Derby na Schalke  04 Mwezi uliopita na kumfanya awe sawa na Yeboah .

Yeboah aliweka rekodi hii akiwa na magoli 96 akiwa amecheza michezo 223 alipokuwa anaichezea Frankfurt katika miaka yake mi tano ndani ya klabu hiyo na haikuwahi kuvunjwa tangu mwaka 1995.

Aubameyang amefikisha magoli 97 katika michezo 143 tangu aanze kuvaa jezi za njano na nyeusi zinazotumiwa na Dortmund tangu atue  msimu wa mwaka 2012-2013.

Safari ya Aubameyang ilianza baada ya kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kwenye historia ya klabu kufunga Hat trick kwenye mchezo wa kwanza wa ufunguzi wa ligi msimu wa  2013-2014 ukiwa ni msimu wake wa pili tangu atue klabuni hapo.

Nakukumbusha kuwa Aubameyang ni mchezaji wa kwanza kutoka Taifa la Gabon kucheza kwenye ligi ya Bundesliga. #Niko_Fair

No comments