SIMBA YAICHAKAZA AFRIKA LYON

Na Said Ally
Kikosi cha timu ya soka ya Simba usiku huu kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi Afrika Lyon katika mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.

Katika mchezo huo wa kirafiki wekundu wa Msimbazi Simba ilitumia wachezaji wake wengi ambao walikuwa hawapati nafasi katika kikosi cha kwanza,baadhi yao wakitoka kikosi cha timu ya vijana ya Simba B.

Simba ilifanikiwa kuibuka na ushindi huo kupitia kwa wachezaji wake John Boko ambae amepachika nyavuni magoli mawili huku mengine yakifungwa na Moses Kitandu pamoja na Kelvin Faru.

No comments