YANGA YAPANGWA NA TIMU KUTOKA SEYCHELLES KLABU BINGWA BARANI AFRIKA

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Tanzania bara timu ya soka ya Yanga wamepangwa kuanza na timu ya St Lous ya Seychelles katika mchezo wa raundi ya kwanza katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika.

Endapo Yanga kama itafanikiwa kufuzu katika mchezo huo wa raundi ya kwanza itakuwa na kibarua kingine cha kucheza na mshindi kati ya El Merreikh ya Sudani au Township Rollers ya Botswana.

Yanga imefanikiwa kucheza kombe la klabu bingwa barani Afrika baada ya kuwa mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara msimu wa mwaka 2017/18.

No comments