YANGA YAANZA MCHAKATO WA MABADILIKO YA UENDESHAJI WA TIMU

Uongozi wa klabu ya Yanga leo hii umetangaza rasmi kuanza mchakato wa mabadiliko ya uendeshaji wa timu kwenda katika mfumo wa Hisa ambapo klabu itamiliki hisa za asilimia 51 huku hisa asilimia 49 zikienda kwa wawekezaji.

Katibu mkuu wa klabu ya Yanga Charse Boniphace Mkwasa alisema kwamba katika kikao cha kamati ya utendaji kilichoketi siku ya jumatano ya tarehe 13 kwa pamoja wajumbe walikubaliana kwa pamoja kuanza mchakato huo kwa kuwa katiba ya Yanga inaruhusu kufanya hivyo.

Alisema kwamba kwa kutambua uzito wa jambo hilo kwa sasa imeundwa kamati maalumu ambayo itakuwa na kazi moja ya kutathmini thamani ya klabu ya Yanga kabla ya kuingia katika mchakato huo.

Hata hivyo aliongeza kwa kusema kwamba swala hilo pia litajadiliwa katika mkutano mkuu wa wanachama ambao ndio wenye mamlaka ya klabu  ya Yanga

No comments