NGASA AJIUNGA RASMI NA NDANDA FC

Na Said Ally
Baada ya kuachwa na klabu ya Mbeya City kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa,mchezaji Mrisho Khalifan Ngasa amejiunga rasmi na klabu ya Ndanda FC kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo katika ligi kuu ya Tanzania bara na michuano ya kombe la FA.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook klabu ya Ndanda imeandika ujumbe wa kumkaribisha Ngasa katika klabu hiyo ya mkoani Mtwara.

Mbali na Ngasa pia klabu hiyo imekamilisha usajili wa mchezaji Ame Ally "Zungu"ambae nae ataungana na Ngasa kwa ajili ya kuwatumikia Wanakuchele hao.

No comments