MSHAMBULIAJI MPYA AZAM FC AANZA KUCHEKA NA NYAVU

KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imetoka sare ya bao 1-1 na Friends Ranger katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenue Uwanja wa Azam Complex usiku wa jana.
Ilikuwa ni siku nzuri kwa mshambuliaji mpya wa timu hiyo Bernard Arthur, aliyekuwa akicheza mechi yake ya kwanza tokea asajiliwe akitokea Liberty Professional ya Ghana baada ya kufunga bao la kusawazisha dakika ya 68.
Mpira huoa ulikuwa ni mkali sana ambapo Azam FC ilicheza vema kipindi cha pili baada ya mabadiliko ya kuingia winga Enock Atta, kiungo Frank Domayo na mshambuliaji Wazir Junior.
Friends Ranger ilijipatia bao lake dakika ya 65 kupitia kwa Mau Gola kufuatia uzembe uliofanyika kwenye safu ya ulinzi ya Azam FC kabla ya dakika tatu baadaye matajiri hao kusawazisha.
Azam FC iliutumia mchezo huo kama sehemu ya kuwapa ushindani wachezaji wake kutokana na kusimama kwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) kupisha michuano ya Kombe la Chalenji inayoendelea nchini Kenya.

No comments