SIMBA YAKAMILISHA USAJILLI WA ASANTE KWASI YAACHANA RASMI NA MAVUGO


Na Said Ally
Klabu ya Simba imefanikiwa kukamilisha usajili wa mchezaji Asante Kwasi, katika dadika za mwisho kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa rasmi hapo jana.

Awali usajili wake ulionekana kukwama baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa mchezaji huyo bado angali na mkataba na klabu ya Lipuili FC.

Mbali na usajili huo pia Simba imekamilisha usajili mshambuliaji kutoka Zambia, Antonio Dayo Domingues.

Aidha imeelezwa kuwa klabu ya Simba imempa kandarasi mchezaji Jonas Sakuhawa kutoka nchini Zambia ambae amekamilisha usajili wa wachezaji watatu wa kigeni katika dirisha dogo la usajili hapo jana.

Hata hivyo taarifa za ndani zinaeleza kuwa klabu hiyo imeachana rasmi na wachezaji wake wa kigeni watatu ambao ni beki Method Mwanjali,Nicholas Gyani na Laudit Mavugo.

Kwa taarifa zaidi endelea kufuatilia MWANDIKE BLOGSPOT.

No comments