WAPINZANI WA SIMBA NA YANGA KUFAHAMIKA KESHO

Na Said Ally
Shirikisho la soka barani Afrika CAF,hapo kesho linataraji kupanga ratiba ya michuano ya kombe la klabu bingwa barani Afrika pamoja na michuano ya kombe la Shirikisho.

Klabu za Simba na Yanga hapo kesho zitafahamu wapinzani wao katika ushiriki wa michuano ya kimataifa kwa ngazi ya vilabu ambayo inaandaliwa na CAF.

Yanga kwa upande wao watashiriki michuano ya klabu bingwa barani Afrika baada ya kuwa mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara wakati Simba kwa upande wao watacheza kombe la shirikisho baada ya kuwa mabingwa wa kombe la FA.

Hata hivyo shirikisho hilo barani Afrika hapo kesho linataraji kupanga ratiba mbalimbali ya michuano inayoandaliwa na shirikisho hilo ikiwemo michuano ya vijana walio na umri wa miaka chini ya 20.

No comments