SIMBA YAPANGWA NA TIMU KUTOKA DJIBOUT KOMBE LA SHIRIKISHO BARANI AFRIKA

Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika timu ya soka ya Simba imepangwa kuanza na timu ya Gendermerie Tnale ya Djibout katika mchezo wa raundi ya awali ya kombe la shirikisho barani Afrika.

Endapo kama wekundu hao wa msimbazi watafuzu katika mchezo huo wa raundi ya awali basi wakuwa na kibarua kingine cha kucheza na mshindi kati ya El Masry ya Misri au Green Button Aloes ya Zambia.

Simba imefanikiwa kupata nafasi ya kucheza kombe la shirikisho barani Afrika baada ya kuwa mabingwa wa kombe la Azam Sports Federation.

No comments