MOURINHO KUENDELEA KUPAKI BASI MBELE YA LIVERPOOL

Mdau mkubwa wa LIVERPOOL KENNY DALGLISH amesema MANCHESTER UNITED itakapopambana na LIVERPOOL Jumamosi hii kuna uwezekano mkubwa JOSE MOURINHO akatumia staili yake ya kupaki basi ili kujihakikishia ushindi.

Amesema kuwa MAN UNITED imekuwa ikifanya vizuri hivi sasa katika michezo yake ambapo katika ligi kuu ya ENGLAND imefunga mabao 21 katika michezo yake saba iliyocheza ikiwa sawa na MANCHESTER CITY.

Hata hivyo DALGISH amesema pamoja ya MAN UNITED kutumia staili ya kujihami dhidi ya vijana wa JURGEN KLOPP wanaocheza mpira wa kushambulia huenda mchezo huo ukaishia bila kupatikana magoli.

MOURINHO amekuwa akitumia staili ya kujilinda kwa muda mrefu na katika staili hiyo amepata mafanikio akiwa na timu mbalimbali japokuwa mbinu hiyo inawakwaza mashabiki wa soka kwa maelezo kuwa inapunguza ladha ya soka uwanjani.

MAN UNITED siku ya Jumamosi itakuwa makini zaidi kwa kuwa tangu ianze ligi kuu ya ENGLAND msimu huu itakuwa sasa inakutana na moja ya timu bora sita za ligi kuu hiyo.

No comments