MTIBWA SUGAR WAPANAGA KUWASILI NA NDEGE JIJINI DAR ES SALAAM

Uongozi wa timu ya Mtibwa Sugar ya Manungu Turiani mkoani Morogoro umesema kwamba kikosi chao bado kipo katika mashamba ya miwa kikiendelea na mazoezi kwa ajili ya kujiwinda na pambano lao dhidi ya Simba hapo siku ya jumapili.

Msemaji wa Mtibwa Sugar,Thobias Kifaru amesema kwamba dhamira yao ni kupata ushindi kwenye pambano hilo ili warejee kileleni kwenye msimamo wa ligi.

Aidha Kifaru alisema kwamba kikosi hicho huenda kikawasili jijini Dar es salaam kwa usafiri wa ndege siku hiyo hiyo ya mchezo utakaopigwa kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Kifaru alisema kwamba Mtibwa Sugar ina uwezo wa kukisafirisha kikosi hicho kwa ndege kwani wana uwezo wa kufanya hivyo.

No comments