BAADA YA KUFUZU KOMBE LA DUNIA RAIS WA PANNAMA ATANGAZA SIKU KUU

Rais wa PANAMA leo ametangaza ni siku ya mapumziko kwa Taifa hilo baada ya timu ya Taifa kufuzu kushiriki fainali ya Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza hapo mwakani nchini URUSI.

Rais huyo alisema vijana wake imefanya jambo la historia kubwa kwa nchi hiyo hivyo wananchi hawana budi kufurahia na kujiweka sawa kwa ajili ya kuipa nguvu timu yao katika fainali za kombe la dunia hapo mwakani.

Kocha wa PANAMA jana usiku katika mchezo huo dhidi ya COSTA RICA timu hizo zimekwenda sare ya bao 1 kwa 1.

PANAMA hawakutegemea kupata nafasi hiyo kwani walitakiwa kupata matokea mazuri huku timu za MAREKANI na MEXICO zifungwe na ndicho kilichotokea  hapo jana, na hivyo PANAMA kupata bahati hiyo ya mtende kuota jangwani.

No comments