MCHEZAJI YANGA AMKINGIA KIFUA GEORGE LWANDAMINA

Mchezaji wa zamani wa timu ya Yanga,Said Maulid amelikingia kifua benchi la ufundi la klabu hiyo linaloongozwa na kocha George Lwandamina kuwa kwa kipindi hiki hawapaswi kulaumiwa kutokana na mwenendo wa timu hiyo.

Maulid ameiambia MWANDIKE.BLOGSPOT.COM kwamba kumekua na mashabiki wa klabu ya Yanga wakiponda uwezo wa kocha George Lwandamina na msaidizi wake Shadrack Nsajigwa kuwa hawastahili kuwepo katika klabu hiyo.

Alisema kwamba mashabiki wanapaswa kuendelea kuwa na subra ili kuwapa muda makocha hao kwani ana imani wana uwezo wa kutosha wa kuifikisha Yanga pale wanapopahitaji.

Aidha aliongeza kwa kusema kwamba mashabiki pia wanatakiwa kutambua kuwa  makocha hao hawana muda mrefu katika kikosi hicho pia ukilinganisha na ukata wa kifedha uliopo ndani ya timu unawapa wakati mgumu kutimiza malengo yao.

Yanga kwa sasa ipo katika nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi kuu ya Tanzania bara ikiwa na alama 9 baada ya kucheza mechi tano.

No comments