YANGA YASHIKANI USUKANI WA LIGI KUU



Timu ya soka ya Yanga imefanikiwa kukamata usukani wa ligi kuu ya Tanzania bara,baada ya jioni hii kufanikiwa kuibuka na ushindi wa jumla ya 2-1 dhidi ya Kagera Sugar.

Kufuatia ushindi huo Yanga imefikisha jumla ya pointi 12 sawa na klabu ya Azam FC ambao nao wana alama 12 lakini mabingwa hao watetezi wako kileleni kwa uwiano mzuri wa magoli ya kushinda.

Yanga ilijipati uongozi wa ligi katika pambano hilo lililokua na ushindani wa hali ya juu kupitia kwa washambuliaji wake Obrey Chirwa na Ibrahim Ajibu Migomba.

No comments