KAGERA SUGAR WAPO KAMILI KUWAVAA YANGA

Uongozi wa timu ya Kagera Sugar umesema kwamba kikosi chao kimejipanga vyema kuwakabili Yanga hapo kesho katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara.

Kocha msaidizi wa Kagera Sugar,Ally Jangalu amesema kwamba dhamira yao kuu ni kushinda pambano hilo litakalopigwa kwenye uwanja Kaitaba mkoani humo kwani tangu kuanza kwa ligi hawajapata matokeo mazuri.

Jangalu alisema kwamba hadi kufikia jioni ya leo katika kikosi hakuna mchezaji aliye majeruhi,hivyo anaamini hilo ni jambo la faraja litakalowapa nafasi benchi la ufundi kuchagua mchezaji watakaemuhitaji kwenye pambano hilo.

No comments