ARJEN ROBBEN ASTAAFU SOKA

Mchezaji nyota wa timu ya Taifa ya UHOLANZI na BAYERN MUNICH ya UJERUMANI ARJEN ROBBEN amestaafu soka la kimataifa jana huku timu yake ikishindwa kufuzu fainali ya kombe la dunia pamoja na kupata ushindi wa mabao 2 kwa 0 yaliyofungwa na nyota huyo.

ROBBEN amestaafu kucheza soka la kimataifa baada ya kuichezea timu ya nchi yake ya UHOLANZI kwa miaka 14.

ROBBEN anashika nafasi na nne kwa kupachika mabao kwa nchi yake ambapo amefunga mabao 37 akilingana na mchezaji mwingine mstaafu wa nchi hiyo DENNIS BERGKAMP.
Mchezaji wengine wa UHOLANZI walioshika nafasi za juu kwa ufungaji ni ROBIN VAN PERSIE aliyefunga mabao 50, KLAAS-JAN HANTELAAR aliyefunga mabao 42 na PATRICK KLAIVET.

ROBBEN amestaafu jana huku akishiriki katika timu ya taifa mara 96 kati ya michezo 189.

No comments