MAREKANI YAWEKA HISTORIA BAADA YA MIAKA 32

MAREKANI imeangukia nafasi ya tano  na kushindwa kufuzu fainali za kombe la dunia baada ya kupata kibano kutoka kwa TRINIDAD na TOBAGO.

Kwa MAREKANI ni mara ya kwanza katika miaka 32 kukosa kushiriki katika fainali za kombe la dunia.

Wachezaji na wapenzi wa soka nchini MAREKANI kwa mara ya kwanza tangu 1986 watashuhudia timu za nchi nyingine katika luninga na mitandao fainali za kombe la dunia hapo mwakani.


Wakati viongozi, wachezaji nyota wa zamani, na wapenda soka wa MAREKANI wamekuwa na kilio cha ajabu tangu jana usiku wenzao wa PANAMA na HONDURAS wakifurahi na tabasamu za hali ya juu zimetawala katika nchi zao.

No comments