YAYA TOURE AITAKA FIFA KUKABILIANA NA UBAGUZI

Kiungo wa kati wa MANCHESTER CITY YAYA TOURE anasema kuwa kombe la dunia la mwaka ujao linaweza kufanikiwa au kutofanikiwa kwa kiasi kikubwa endapo kutakuwa na ubaguzi wa rangi.

TOURE mwenye umri wa miaka 34 amekabiliwa na matamshi ya ubaguzi wa rangi wakati City ilipocheza dhidi ya CSKA Moscow katika kombe la vilabu bingwa nchini Urusi 2013.

Anataka kuisaidia Fifa na serikali ya Urusi kukabiliana na tatizo hilo kabla ya michuano hiyo kuanza rasmi.


Mwezi uliopita, LIVERPOOL imelalamika kwa UEFA kuhusu madai ya matamshi ya ubaguzi wa rangi yaliomlenga winga BOBBY ADEKANYE wakati wa mechi ya kombe la UEFA upande wa vijana katika uwanja wa SPARTAK MOSCOW.

No comments