ALLY BUSHIRI KUMFUTA KAZI KOCHA WA MWADUI FC

Na Sleiman Ussi,Zanzibar
Aliyekua kocha wa timu ya Mwadui FC inayoshiriki ligi kuu ya Tanzania bara,Ally Bushiri huenda akarejea katika kikosi cha timu hiyo baada ya kuwepo kwa mazungumzo kwa pande zote mbili.

Bushiri ameiambia MWANDIKE.BLOGSPOT.COM kwamba alienguliwa katika kikosi cha timu hiyo msimu uliopita kutokana na kocha msaidizi wa klabu hiyo kueneza chuki juu yake kwa uongozi ikiwemo kuwaambia viongozi kuwa hana uwezo wa kushinda mechi za ugenini.

"Niseme tu nilipata baadhi ya salamu ama niseme simu kwamba kuna mipango hiyo ya kutakiwa kurudi katika kufundisha timu ya Mwadui FC,lakini bado kidogo kuna mkanganyiko fulani na mkanganyiko huu niwe muwazi kwamba sababu ni yule mwalimu msaidizi ambae nilikua nae pale ndio chanzo kikubwa cha mimi kufutwa kazi kwa sababu ilionekana hakupendeza na utendaji wangu wa kazi" alisema Bushiri.

Hata hivyo alisema kwamba anaweza kurejea katika timu hiyo lakini amewaambia viongozi wa Mwadui FC kwanza wachukue jukumu la kumfuta kazi aliyekua kocha msaidizi wake alipokua anaifundisha timu hiyo.

No comments