CITY WAENDELEA KUWANIA SAINI YA LIONEL MESSI

MANCHESTER CITY imetangaza kumwania kumsajili nyota wa ARGENTIANA na BARCELONA LIONEL MESSI, lakini SERGIO AGUERO amesema haoni ni rahisi kufanya hivyo.

AGUERO amesema kuwa angependa acheze na LIONEL MESSI  wakiwa MAN CITY lakini ni vigumu kumshawishi mchezaji huyo nyota wa BARCA kwa sasa kutua CITY.

Ameongeza kuwa MESSI hivi sasa ni alama ya BARCELONA, kumwondoa katika klabu hiyo itakuwa ni shughuli pevu ambayo itagharimu kwa kiasi kikubwa kwa namna mbalimbali.

Habari za uwezekano wa MESSI kuondoka BARCELONA zimekuwa zikisemwa kwa mwezi mzima sasa, na Rais  wa BARCELONA JOSEP MARIA BARTOMEU amedai kuwa suala la MESSI kusaini mkataba mpya tayari limeshafanyiwa kazi na bado kutangazwa tu rasmi, lakini jambo hilo limeendelea kuchukua nafasi kwamba huenda MESSI akaondoka. 

No comments