DIEGO SIMEONE KUBADILI REKODI

ATLETICO MADRID kesho itaikaribisha BARCELONA kwa mara ya kwanza tangu Ligi kuu ya HISPANIA LA LIGA ianze msimu huu huku mashabiki wakiwa hamu kubwa ya kushuhudia pambano hilo linalotegemewa kuwa burudani ya kukonga roho.

Mashabiki wa soka wamekuwa wakijadili endapo kocha DIEGO SIMEONE ataibadilisha rekodi yake kwa kuipiga BARCELONA hapo kesho.

BARCELONA mpaka sasa inaongoza msimamo wa LA LIGA akiwa na pointi tano zaidi ya SEVILLA inayoshika nafasi ya pili.


Katika LA LIGA timu za ATLETICO MADRID, BARCELONA na VALENCIA hajapoteza mchezo hata mmoja hadi sasa.

No comments