KOCHA WA COLOMBIA AMSHUKURU DUVAN ZAPATA

Baada ya COLOMBIA kufuzu fainali ya Kombe la dunia, kocha mkuu wa timu hiyo JOSE PEKERMAN amemshukuru mchezaji DUVAN ZAPATA kwa mchango wake mkubwa katika ushindi huo.

PEKERMAN amemtaja mchezaji huyo kwa jina bila kuangalia timu mzima kwa kazi waliyofanya kwa pamoja kwa kuiwezesha COLOMBIA kuwapa sare ya bao 1 kwa 1 dhidi ya PERU na kutinga fainali ya kombe la dunia hapo mwakani.

Kocha huyo alisema ZAPATA amefanya mambo makubwa katika mchezo huo na ilikuwa sio rahisi kwa COLOMBIA kuweza kupata bao hilo dhidi ya PERU.

Ameongeza kuwa mchezaji huyo ni lulu kwa COLOMBIA na nguvu na uwezo wake ni muhimu sana kwa timu  yake katika michuano ya fainali ya kombe la dunia ijayo.

No comments