DONALD NGOMA AWAFUATA KAGERA SUGAR

Kikosi cha timu ya Yanga hapo kesho asubuhi kinataraji kuelekea mjini Bukoba kwa ajili ya kujiwinda na pambano lao la ligi kuu ya Tanzania bara dhidi ya Kagera Sugar,mchezo unaoatarajiwa kupigwa mkoani Kagera siku ya jumamosi ya octoba 14 mwaka huu.

Afisa Habari wa Yanga Dismas Teni ameiambia MWANDIKE.BLOGSPOT.COM kwamba katika msafara huo watakosekana wachezaji watatu akiwemo Thabani Kamusoko aliye na maumivu ya kifundo cha mguu.

Dismas alisema kwamba wachezaji wengine ambao hawataambatana na timu ni mlinda mlango Ramadhani Kabwili na Mussa Said ambao hawa kwa pamoja wote wapo kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Ngorongoro Heroes.

Alisema kwamba katika mchezo huo pia wataambatana na mchezaji Donald Ngoma ambae alikuwa majeruhi baada ya kuumia katika mechi yao iliyopita dhidi ya Mtibwa Sugar.

Hata hivyo Ten aliongeza kwa kusema kwamba wameamua kwenda na kikosi kipana kwa sababu mbali na mchezo huo pia watacheza mechi nyingine ya ligi dhidi ya Stend United itakayopigwa mkoani Shinyanga.

No comments