FRIENDS RENGERS WAWASIFU WAAMUZI

Baada ya kulazimishwa sale ya 1-1 na kikosi cha Afrika Lyon katika mchezo wa ligi daraja la kwanza,uongozi wa timu ya Friends Rengers umesema kwamba hadi kufikia sasa wameridhishwa na kiwango cha waamuzi wa mechi zao.

Meneja wa timu hiyo,Shabani Masila alisema kwamba waamuzi wa msimu huu ambao wamechezesha mechi zao wanastahili sifa kwani wameonyesha mabadiliko makubwa tofauti na msimu uliopita.

Masila alisema kwamba endapo kama waamuzi hao wataendelea hivyo kama walivyofanya katika mechi nne walizocheza anaaamini Friends Rengers itapata nafasi ya kucheza ligi kuu ya Tanzania bara msimu ujao.

No comments