PAUL MERSON ASEMA REDKNAPP NI BORA KULIKO WENGER

Mchezaji wa zamani wa ARSENAL na PORTMOUTH PAUL MERSON amesema kiufundi kocha HARRY REDKNAPP yuko vizuri zaidi ya ARSENE WENGER.

MERSON ana amini kuwa ARSENAL ingekuwa bingwa wa ligi kuu ENGLAND endapo WENGER angetumia njia ya kiufundi ya uwanjani anayotumia kocha wa TOTTENHAM HARRY REDKNAPP.


ARSENAL haijapata ubingwa wa ligi kuu ENGLAND tangu msimu wa 2003-04 na sasa WENGER yuko katika presha kubwa kutoka kwa mashabiki wa timu hiyo ambao wana kiu ya kuona timu yao inapata ubingwa.

No comments