ADRIANO ATAKA KUSTAAFU KWA KISHINDO

Mshambuliaji nyota wa zamani wa BRAZIL ADRIANO mwenye umri wa miaka 35 anataka kustaafu kabisa soka kwa kishindo hapo mwakani.

ADRIANO amesema shughuli bado inaendelea na ameweka wazi mipango yake ya kurudi katika kandanda.

Nyota huyo wa zamani wa BRAZIL hajacheza tangu wakati akiwa na MIAMI UNITED mwaka jana lakini amepanga kucheza  Klabu Bingwa AMERIKA na Kombe vilabu Shirikishi hapo mwakani.

RONALDO DI LIMA nyota wa BRAZIL alifanikiwa kurudi katika soka baada ya kukaa nje ya soka kwa muda mrefu, lakini ADRIAN amekuwa akishindwa kufanya hivyo mara kwa mara kutokana na kukabiliwa na changamoto mbalimbali katika maisha.


ADRIAN ambaye amefanikiwa kuchukua ubingwa akiwa na Ligi ya ITALIA na INTER MILAN, amefunga mabao 74 katika mashindano mbalimbali.

Mchezaji huyo pia amecheza soka akiwa na Klabu za AC ROMA, FIORENTINA, PARMA, FLAMENGO, CORINTIANS. SAO PAULO na ATLETICO PARANAENSE.

No comments