COASTAL UNION WAIACHIE TFF JUU YA MADAI YA FEDHA ZA JUMA MAHADHI

Uongozi wa timu ya Coastal Union ya mkoani Tanga umesema kwamba kwa sasa swala zima la madai ya fedha zao za wachezaji ambao wamesajiwa na vilabu vingine jambo hilo wameliacha kwa TFF ili walifanyie kazi nao wapewe haki yao.

Akiongea na MWANDIKE.BLOGSPORT,kaimu katibu mkuu wa klabu hiyo Salum Bawazir amesema kwamba jambo hilo wameliacha kwa TFF na wanaamini fedha zao ambazo wanazidai kwa wachezaji hao zitapatikana.

Amesema kwamba klabu hiyo inazidai klabu mbalimbali za Tanzania kuhusiana na ada ya uhamisho wa wachezaji sambamba na fedha za usajili kwa wachezaji ambao wamevunja mikataba yao.

Bawaziri amedai kua miongoni mwa klabu ambazo wanazidai ni pamoja na timu ya Yanga juu ya mchezaji Juma Mahadhi ambapo klabu ya Yanga inadaiwa fedha za ada ya uhamisho wa kuidhinishwa kuitumikia timu hiyo kwa msimu huu.

Aidha amesema kwamba pia zipo klabu za Simba,Mbeya City pamoja na klabu nyingine ambazo kwa namna moja zimehusika kuchukua wachezaji wa timu hiyo iliyo kwenye maandalizi ya kurejea katika ligi kuu ya Tanzania bara.

No comments