MWAISABULAH ASEMA LIGI YA MSIMU HUU INA UPINZANI MKUBWA
Mchambuzi wa soka pia akiwa mwalimu wa mpira wa miguu hapa nchini Kenny Mwaisabulah amesema kwamba ligi kuu ya Tanzania bara ya msimu ni ngumu tofauti na miaka mingine kutokana na timu mbalimbali kujipanga kikamilifu.
Mwaisabula amesema kwamba katika mechi ambazo amepata kuzishuhudia ameona jinsi gani timu zilivojipanga licha ya kuwepo na mapungufu kwa baadhi ya wachezaji na timu husika kwa ujumla.
Amesema kwamba timu za Azam,Yanga na Simba zitaendelea kutamba kutokana na uimara uliopo kwenye vikosi vyao ingawa nao watakumbana na changamoto kubwa hususani kwa timu ya Yanga ambayo mfumo wa wachezaji wao unatambulika na timunyingine hivyo kuwa rahisi kuwazuia.
Aidha amesema kwamba timu ya Mbao FC ya mkoani Mwanzan inakabiliwa na changamoto kubwa katika ligi kuu kwa kua timu hiyo haikua tayari kushiriki msimu huu kutokana na maandalizi yao kua finyu.
Amesema kwamba ingawa viongozi wa Mbao wanajinasibu kufanya vizuri msimu huu lkn wana changamoto kubwa ya kupata matokeo mazuri hasa kwenye mzunguko wa pili ambao kila timu itakua na kazi kubwa ya kusaka alama tatu.
"Hata kama viongozi wa mbao wanazungumza kwamba watafanya vizuri kwenye mechi zijazo lakini ukweli timu hiyo ina kazi kubwa hasa katika mzunguko wa pili ambapo kila timu itahitaji pointi tatu ili isishuke daraja ama itwae ubingwa"alisema Mwaisabula
Post a Comment