MKWASA KUITEMA TAIFA STARS





Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars,Charse Boniphace Mkwasa amesema kwamba hatarajii kama ataendelea kusalia kukinoa kikosi cha timu ya Taifa mara baada ya mkataba wake unaoshia mwezi wa tatu mwaka hapo mwakani kumalizika.

Mkwasa amesema kwamba kwa muda wake ambao amekaa na timu ameona inatosha na jukumu hilo ni vyema awaachie wengine ambao nao huenda wakawa na mbinu mpya zitakazosaidia Stars kufanya vizuri kwenye michuano mbalimbali huku yeye akibaki kua kama mshauri.

Amesema kwamba kwa upande wake amekumbana na changamoto mbalimbali ndani ya timu hiyo lkn kwa juhudi zake akishirikia na wenzake pamoja na wachezaji wamejalibu kufanya kile ambacho wamekiweza kwa wakati huu.

“Siwezi kusema kama nitaendelea kuwepo kwenye timu ya taifa au nitaacha pale  mkataba wangu utakapoisha lakini ki ukweli hapa nilipofika panatosha mkataba ukiisha umeisha,ngoja tuwaachie wengine waongoze sijui atakua mzungu au mzawa”alisema Mkwasa.

No comments