MBAO FC YAWATOA HOFU MASHABIKI WAO KUHUSU MWENENDO WA LIGI

 Baada ya kushindwa kufanya vyema kwenye mechi tatu za ligi kuu ya Tanzania bara,uongozi wa klabu ya Mbao FC ya Ilemela kutoka jijini Mwanza umesema kwamba kikosi cha timu hiyo kinataraji kuanza safari siku ya jumamosi kuelekea jijini Dar es salaam kwa ajili ya pambano lao dhidi ya Afrika Lyon.

Msemaji wa timu hiyo,Christian Malinzi amesema kwamba kwa sasa kocha mkuu wa klabu hiyo anajalibu kuyafanyia kazi mapungufu ambayo yameoneka kujitokeza hasa kwenye safu ya ulinzi.

Amesema kwamba licha ya kufungwa mechi mbili mfululizo tena wakiwa nyumbani bado wana amini watafanya vizuri msimu huu na kusalia katika ligi kuu ya Tanzania bara.

"Nawaomba mashabiki wa timu yetu wasiwe na wasiwasi wowote baada ya kufungwa mechi mbili waamini Mbao itafanya vizuri kwani ligi ndio kwanza imeanza" alisema Malinzi

No comments