PAN AFRIKA YAITISHA MKUTANO MKUU WA WANACHAMA



Uongozi wa klabu ya Pan Afrika ya jijini Dar es salaam ambayo inashiriki ligi daraja la pili ngazi ya mkoa,umesema kwamba baada ya kumaliza mgogoro uliopo kwa muda mrefu ndani ya timu hiyo kwa sasa wamejipanga kufanya mkutano mkuu wa wanachama ambao unataraji kufanyika siku ya tarehe 11 ya mwezi wa 9 mwaka huu.

Katibu wa timu hiyo Sad Mateo amesema kwamba mkutano huo unaotaraji kufanyika kwenye uwanja wa Taifa una ajenda saba ambazo dhumuni kubwa la mkutano huo ni kujadili maswala mbalimbali ya klabu ambayo kwa muda mrefu tangu iliposhuka katika ligi kuu ya Tanzania bara imekua ikisua sua na kupelekea kua na migogoro ya mara kwa mara.

Amesema kwamba wanachama wa klabu hiyo ambao hai na wasio hai wanapaswa kulipa ada zao mapema ili wawepo kwenye mkutano huo huku pia nao wanachama wapya ambao wanahitaji kujiunga na timu hiyo ni vyema nao wakafuata taratibu husika mapema za kujiunga kabla ya mkutano huo.

No comments