NAPE NA MALINZI WAWAPA HOFU WANAOTAKA KUMILIKI TIMU ZA SIMBA NA YANGA
Serikali kupitia kwa Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Nape Nnauye imesema kwamba hawatakubaliana na maamuzi ya wanachama wa vilabu vya Simba na Yanga ama klabu yeyote ambayo inataka kuingia kwenye mfumo wa mabadiliko pasipo kupata vigezo kamili ambavyo wataviridhia wao kuviruhusu vilabu viingie kwenye mfumo huo.
Akiongea mbele ya waandishi wa Habari leo hii,Nape amesema kwamba kumekua na mjadala mkubwa hasa kwa vilabu vya Simba na Yanga juu ya mfumo wa mabadiliko ya kiuendashiji lkn kumekua hakuna maelezo ya kutosha ambayo yanaonyesha kutoleta kwa mvuragano hapo baadae.
Amesema kwamba ni vyema vilabu hivyo vikajifanyia tasmini kabla ya kuingia kwenye mifumo hiyo ikiwemo kupata ushauri kutoka kwao ambapo kwa mujibu wa taarifa yake amedai kua wako radhi kuwasidia kwenye jambo hilo.
Kwa upande wake shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF limesema kwamba hawatakubaliana na maamuzi ya vilabu hivyo juu ya mabadiliko ya mfumo endapo yule anaepewa jukumu la kumiliki timu hana sifa.
Akiongea mbele ya waandishi wa Habari Raisi wa TFF,Jamali Malinzi amesema kwamba klabu zinapaswa kufahamu juu ya jambo hilo kwamba kwa sheria za FIFA kuna kipengele cha kufahamu sifa ya anaetaka kumiliki timu.
Post a Comment