MALALE HAMSINI ATAMBA KUPATA USHINDI WA KWANZA MBELE YA NDUGU ZAO

Uongozi wa klabu ya JKT Ruvu ya mkoani Pwani umesema kwamba kwa sasa wapo katika maandazi ya mwisho mwisho kuelekea kwenye pambano lao la ligi kuu ya Tanzania bara dhidi ya ndugu zao Ruvu Shooting hapo kesho katika mechi itakayopigwa kwenye uwanja wa mabatini.

Kocha mkuu wa klabu hiyo Malale Hamsini ameiambia MWANDIKE.BLOGSPORT kwamba katika pambano hilo linalotaraji kupigwa siku ya jumamosi wanataraji kumkosa mchezaji wao Michael Aidani ambae ni majeruhi.

"Namshukuru mungu wachezaji wote wapo vizuri isipokua Michael Aidani ambae ni majeruhi lkn naamini kwenye mechi hiyo tutafanya vizuri huku tukitaraji kupata ushindi wa kwanza baada ya mechi mbili kutoka sale"alisema Malale Hamsini.

Amesema kwamba anaamini pambano hilo litakua gumu kutokana na upinzani uliopo baina ya timu hizo lkn jambo hilo halitakua na kikwazo kwake kutochomoza na ushindi.


No comments