MTIBWA SUGAR WATAMBA KUIFUNGA SIMBA JUMAPILI

Uongozi wa timu ya Mtibwa Sugar ya Manungu Turiani mkoani Morogoro,umesema kwamba kikosi cha timu hiyo kinaendelea na maandalizi ya kujiwinda na mchezo wao ujao dhidi ya Simba katika mechi inayotaraji kupigwa siku ya jumapili kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Msemaji wa timu hiyo Tobiasi Kifaru ameiambia MWANDIKE.BLOGSPORT kwamba wanaamini kwenye pambano hilo watapata matokeo mazuri mbele ya Simba hii inatokana na ubora wa kikosi chao kinachofundishwa na kocha Salum Mayanga.

Kifaru amesema kwamba Simba ni timu ya kawaida na haina tofauti na Mtibwa Sugar hivyo kwao wana matumaini makubwa ya kuzoa pointi tatu muhimu.

"Mtibwa Sugar na Simba viwango vyao vinalingana na ndio maana unaona kila mara viongozi wa Simba wanapigania kuchukua wachezaji wetu,hii inaonyesha jinsi gani tulivyo bora hivyo kuelekea mechi hiyo kwetu hatuna presha"alisema Kifaru.

Hata hivyo Kifaru amesema kwamba kuelekea kwenye mechi hiyo wanataraji kumkosa mlinda mlango wao namba moja Said Mohamed ambae ni majeruhi.

No comments