MOROGORO NA ILALA KUCHEZA FAINALI YA MICHUANO YA AIRTEL RISING STAR


Timu ya mkoa wa Morogoro imefanikiwa kutinga hatua ya Fainali ya michuano ya Airtel Rising Star baada ya hii leo kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 mbele ya timu ya Temeke katika mechi ambayo imechezwa kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.

Morogoro ilikua timu ya kwanza kuingia fainali kwa upande wa wavulana baada kupata ushindi huo katika mechi iliyomalizika majira ya saa sita mchana kwa saa za hapa nyumbani ambapo mechi hiyo ilisheheni ushindani wa hali juu kwa kila timu.

Kwa matokeo hayo timu ya Morogoro sasa itamenyana na Ilala katika fainali inayotaraji kupigwa hapo kesho kwenye uwanja wa Karume baada ya kufanikiwa kuibuka na ushibndi wa jumla ya mabao 2-0 dhidi ya Kinondoni.

Mabao kwa upande wa washindi yamefungwa na Rajabu Ally katika dakika ya 17 huku bao la pili likifungwa na mchezaji Munir Mzee katika dakika ya 65.

Katika hatua nyingine fainali ya michuano hiyo itahitimishwa hapo kesho kwenye uwaja huo wa Karume ambapo waziri wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Khasim Majaliwa akitarajiwa kuwa mgeni rasmi.

Kwa upande wa wasichana timu ya Temeke imefanikiwa kutinga katika hatua ya fainali baada ya kupata ushindi wa jumla ya mabao 4-1 mbele ya Kinondoni,ambapo kwa matokeo hayo sasa Temeke atamenyana na Ilala kwa upande wa wasichana.


No comments