SOPHIA MJEMA AZINDUA RASMI MICHUANO YA AIRTEL RISING STAR KWA NGAZI YA KITAIFA


Michuano ya Airtel Rising Star kwa ngazi ya kitaifa imefunguliwa rasmi leo hii na mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema ambae amechukua jukumu hilo kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paulo Makonda katika uzinduzi uliofanyika kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.

Michuano hiyo ya kuibua vipaji kwa vijana wa Tanzania kwa sasa yameingia kwenye ngazi ya kitaifa baada ya kuhitimisha kwenye ngazi ya mikoa,ambapo kwa sasa kila mkoa utakua na changamoto ya kufanya vizuri katika mashindano hayo yanayotaraji kufika tamati siku ya jumapili ijayo huku Waziri mkuu wa Tanzania Khasim Majaliwa akitarajiwa kua mgeni rasmi katika hitimisho la michuano hiyo kwa mwaka huu.

Akiongea katika ufunguzi wa michuano hiyo mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema amewataka washiriki wa michuano hiyo ya Airtel Rising Star kutambua umuhimu wa mashindano hayo huku wafahamu kua kwa sasa mpira ni ajila hivyo juhudi zao ambazo watakazozionyesha itakua chachu kwao kuonekana na vilabu mbalimbali vya hapa nchini na nje ya nchi.

"Nawasihi nyie vijana mcheze kwa kujituma kwenye mashindano haya ya Airtel Rising Star kwani wadau mbalimbali wanatupia jicho michuano hii ambayo kwa sasa imekua chachu ya maendeleo ya kuibua vipaji"alisema Sophia Mjema.

Michuano ya Airtel Rising Star imekua msada mkubwa kwa Taifa kwani kwa imekua ikiibua vipaji vya wachezaji ambao hua wanakua na msada kwa timu za Taifa mfano mzuri timu ya vijana ya Kilimanjaro Stars ambayo kwa sasa inasaka tiketi ya kucheza fainali za vijana kwa Afrika.

Mikoa ambayo imepata nafasi ya kushiriki msimu huu ni pamoja na  Mwanza,Arusha,Morogoro,Lindi,Mbeya,Temeke,Kinondoni,Ilala pamoja na Zanzibar.

No comments