SIMBA YAJINASIBU KUPATA POINTI TATU MBELE YA RUVU SHOOTING

 Uongozi wa timu ya soka ya Simba umesema kwamba kikosi chao kimejiandaa vyema kuwakabili Ruvu Shooting ya Mkoani Pwani hapo kesho katika mchezo wao wa ligi kuu ya Tanzania bara unaotaraji kupigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Mkuu wa mawasiliano wa klabu hiyo,Haji Manara ameiambia MWANDIKE.BLOGSPORT kwamba wachezaji wote wako vizuri hakuna majeruhi yeyote na kwa sasa wapo kambini jijini Da es salaam mara baada ya kurejea wakitokea mkoani Dodoma ambako walicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Polisi Dodoma.


Manara amewataka mashabiki wa klabu hiyo kuvaa jezi za Simba kwenye mechi hiyo ili kuleta tija na amewatoa hofu kutohofia kauli za msemaji wa Ruvu Shooting Masau Bwire kuhusiana na tambo zake.

"Mimi ni msemaji wa timu kubwa bwana siwezi kushinda na msemaji ambae timu yake haina hata mashabiki 100 wao wasubiri tu kipigo kutoka kwetu kwa timu yenye heshima kubwa barani Afrika" alisema Manara

No comments